Nenda kwa yaliyomo

Ghada Adel

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ghada Adel
Amezaliwa Ghada Adel
Misri
Kazi yake Muigizaji
Ghada Adel
Ghada Adel

Ghada Adel alizaliwa Benghazi, Libya, katika familia ya wafanyakazi wa Misri.[1] Mama yake aliyekuwa Misri pia alikuwa ni dada wa mwigizaji Shams el-baroudi aliyestaafu ambaye ni dada yake kupitia mama yake.[1][2]Mama yake mzazi alifariki akiwa na miaka miwili, hivyo yeye pamoja na ndugu zake waliishi na baba yao pamoja na mke wa pili wa baba yao huko Libya ambapo baba yao alikuwa akifanyia kazi ,ingawa wanatumia likizo yao ya mwishoni mwa mwaka nyumbani kwao Cairo.[3] Pia ana kaka mmoja mkubwa na wadogo zake wa tatu wakike. Alihitimu katika chuo kikuu cha Benghazi baada ya kusoma usimamizi wa biashara. Alianza kama mwanamitindo waki biashara, akiwa na Hany Shaker mnamo 1997 Tekhsary, kisha kuwa mtangazaji wa kipindi katika televisheni Fawazir abyad wa aswad.[4]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Jukumu lake la kwanza lilikuwa katika kipindi cha televisheni cha Zizinya mnamo 1997, na filamu yake ya kwanza ilikuwa ni vichekesho vya asili Saʽidi katika Chuo Kikuu cha Marekani mnamo 1998 na Mohamed Henedi. Aliigiza nafasi kuu katika filamu nyingi, zikiwemo Belyah and his High Mind mwaka wa 2000, El basha telmeez mwaka wa 2004 na Karim Abdel Aziz, Lover Boys mwaka wa 2005 na Hamada Helal, She Made Me Criminal mwaka wa 2006 na Ahmed Helmy na Hassan Hosny, na Ahwak mwaka wa 2015 na Tamer Hosny. Aliigiza pia katika vipindi vingi vya TV, vikiwemo Mabrouk Galak Ala'a mwaka wa 2005 na mwigizaji Hany Ramzy, Dead Heart mwaka wa 2008 na Sherif Mounir na Saraya Abden mwaka wa 2015 akiwa na Qusai Khouli. [5]

Mnamo mwaka 2019, alienda Viral marketing kwenye majukwaa mengi ya mitandao ya kijamii kwa mtazamo wake wa kuthubutu katika Tamasha la Filamu la El Gouna.[6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. بالفيديو: "مذكرات" غادة عادل بالليبي
  2. "شمس البارودي تكشف صلة القرابة التي تجمعها بريم البارودي وغادة عادل | وكالة الرأي الدولية". www.alrai-iq.com. Iliwekwa mnamo 2020-06-30.
  3. مقال نادر كتبت غادة عادل من لندن، حيث اعتادت قضاء رأس السنة مع أولادها وزوجها، لجريدة "الدستور" المصرية, Agosti 2014{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-12-06. Iliwekwa mnamo 2021-10-30.
  5. Ghada Adel The Egyptian Start Stays Young at Heart interview with Enigma magazine in 2012
  6. Ghada Adel Goes Viral for Her Daring Look at GFF, 25 Septemba 2019{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ghada Adel kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.