Nenda kwa yaliyomo

Historia ya Kanisa Katoliki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria

Muundo

Papa: Fransisko
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Liturujia ya Trento Milano Toledo Braga Lyon Canterbury)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Kanisa Katoliki likiwa la zamani (Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki wanashiriki sifa hiyo) na kubwa kuliko madhehebu yote ya Ukristo, historia yake inashika sehemu muhimu ya historia ya Kanisa lote duniani tangu lilipoanza mwaka 30 hivi BK hadi leo.

Baada ya Yesu Kristo kuhubiri na kukusanya wafuasi kati ya Wayahudi wa karne ya 1, hao walitumwa naye duniani kote, hasa wanaume 12 aliowaita Mitume, yaani "waliotumwa".

Waandamizi wao katika uongozi wa Kanisa walianza kuitwa maaskofu, na kati yao yule wa Roma alizidi kushika nafasi ya pekee kwa sababu Mtume Petro alifia dini katika mji huo kutokana na dhuluma dhidi ya Ukristo ambayo ilianzishwa na Kaisari Nero (mwaka 64) na kuendelea kwa kwikwi hadi ilipokomeshwa na Kaisari Konstantino Mkuu aliyetangaza huko Milano uhuru wa dini kwa wananchi