Kemia kichambuzi
Mandhari
![](http://chped.net/https/upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/9/92/Flame_test.jpg/300px-Flame_test.jpg)
Kemia kichambuzi ni tawi la sayansi ya kemia. Inachunguza dutu mbalimbali kwa shabaha ya kujua viwango na hali za kemikali ndani yao.
- uchambuzi stahilifu unachungulia ni kampaundi na elementi gani zilizopo katika dutu; unauliza je dutu hii ni nini? Kuna nini ndani yake?
- uchambuzi wa kiasi unachungulia hizi kampaundi na elementi zinapatikana kwa kiasi gani
- uchambuzi wa muundo unachungulia je molekuli za dutu zimepangwa namna gani, kwa mfano kwa fuwele au namna nyingine