Nenda kwa yaliyomo

Makuria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Neno “Kuria/koria”  (Mukuria/Mokoria) etimolojia yake hasa ni kutoka katika lugha za Kibantu katika lahaja ya Kisimbiti na Kikuria (Kikurya) ambapo neno hilo lilitokana na neno “Okoria” (Okorya) lenye maana ya (Ulaji) ambapo kiasili  neno hilo lilitamkwa kuwa “Mokoria” (Mokorya) kwa maana ya “Mle au Mnaokula”.Katika wingi wao jamii ya watu hao ambao hasa ni walaji wakubwa wa nyama waliitwa “Abhakoria/Abhakuria” (Abhakoria/Abhakurya) yaani watu walaji (Eaters) ambapo kutokana na watu hao hapo kale kuwa na  hulka ya kutisha kwa ukali na haiba  ya maumbo makubwa ya miili yao, waliitwa “Amakoria/Amakuria”(Makoria/Makuria) ikiwa na maana ya “Majitu” (Giants).[1]

Kuanzia karne ya 10 KK hadi karne ya 4 KK Wabantu wa jamii ya Abakuria (Makuria) pamoja na Wasuba kutoka pande za Maziwa Makuu hasa Nyanza (Viktoria Nyanza) walisafiri kupitia mto Nile mweupe hadi Karthoum (Khartoum) na Mashariki ya Kati kufanya kazi za kijeshi kama askari wa kukodiwa katika majeshi ya Waseba wa Kaskazini, Wakushi,Watiro na Waisraeli.[2]

Huko katika Mashariki ya Kati, Watu Wasuba pamoja na Wabantu wa jamii ya “Abakuria” (Makuria) walifika eneo la Mara lenye kuwa na asili ya maji machungu, eneo ambalo kwa lugha ya Kisemitiki katika lahaja ya Kiebrania liliitwa “Mara” maana yake “Machungu”.Maji yenye uchungu yaliyopatikana katika eneo hilo la jagwa katika Mashariki ya Kati  hao Abakuria (Makuria) waliyafananisha na kimiminika kilichotoka kichungu kilichotoka katika utumbo wa  mnyama wa aina ya mbuzi ambao waliuita “Amara” (Mara).

Baada ya kumalizika kwa vita ya Mashariki ya Kati katika karne ya  4 KK , askari  hao mamluki wa Kisuba na Kikuria walirudi katika nchi ya Kushi (Bara la Afrika) na kuweka makazi yao katika Nubia (Sudani) katika eneo la “Sobat”.Eneo hilo waliloweka makazi yao liliitwa “Sobat” kutokana na kunasibishwa na jina walilopewa askari hao waliokuwa wakirejea kutoka vitani  la “Abasoba” ambalo kwa lugha ya Wabantu wa wakati huo ilimaanisha “Wanaorudi toka vitani au Wanyonyaji”.

Hata hivyo, kutokana na kushamiri kwa vita ya kati ya Warabu na Watu weusi wa pande za Kaskazini mwa bara la Afrika, katika karne ya 15 BK Wabantu hao wa jamii Abakuria (Makuria) walihama na kurejea katika makazi ya mababu wa mbari yao katika eneo la Mara linalopatikana nchini Tanzania ambapo jamii hizo za Wasuba na Wakuria zinaishi kuzunguka ziwa Vikroria katika nchi za Tanzania na Kenya hadi sasa.

Hivyo basi, kutokana na historia ya jamii hii ya Abakuria (Makuria) kuwa watu waaminifu, jasiri na hodari katika medani ya vita, mara tu baada ya uhuru wa iliyokuwa nchi ya Tanganyika katika Afrika ya Mashariki ambayo baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika mwaka 1964 iliitwa Tanzania, Wabantu hao wa jamii ya Abakuria (Makuria) waliendelea kuaminiwa kiasi cha kupewa nafsi za juu katika jeshi la Tanzania.

  1. Maisha Ya Watu Na Wanadamu Anuwai Katika Edeni Ya Tanzania Na Mashariki mwa Dunia, ISBN: 978-9912-40-424-3
  2. Maisha Ya Watu Na Wanadamu Anuwai Katika Edeni Ya Tanzania Na Mashariki mwa Dunia, ISBN:9789912-40-424-3