Nenda kwa yaliyomo

Olena Zelenska

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Zelenska mnamo 2021

Olena Volodymyrivna Zelenska (née Kiyashko ; alizaliwa 6 Februari 1978) ni mwandishi wa skrini wa nchini Ukraini ambaye kwa sasa ni mwanamke wa kwanza wa Ukraini kama mke wa Raisi Volodymyr Zelenskyy . [1] Mnamo Desemba 2019, Zelenska alijumuishwa kati ya Waukraini 100 wenye ushawishi mkubwa katika jarida la Focus, na akachukua nafasi ya 30. [2]

Maisha ya awali na kazi[hariri | hariri chanzo]

Olena Kiyashko alizaliwa huko Kryvyi Rih mnamo 6 Februari 1978. [3] Zelenska alisomea usanifu katika Kitivo cha Uhandisi wa kiraia katika Chuo Kikuu cha Kryvyi Rih National University . Alikua mwandishi wa Kvartal 95 . [4]

Mwanamke wa Kwanza wa Ukraini[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Mei 20, 2019, Zelenska alikua mwanamke wa kwanza wa Ukraini. Tarehe 18 Novemba alionekana kwenye gazeti la Vogue la toleo la Desemba la Kiukreni. Katika mahojiano na gazeti hili, alizungumza juu ya mpango wake wa kwanza wa mageuzi ya lishe katika shule za Ukraini. [5] [6]

Kwa mpango wa Olena Zelenska, marekebisho ya mfumo wa lishe shuleni yalianza na menyu mpya ya shule iliyoandaliwa na mpishi Ievgen Klopotenko wa CultFood. Marekebisho hayo yalikua ni magumu, kutokana kwa kuboresha kwa ubora wa lishe ya chakula, na usalama wa chakula hadi utoaji wa rasilimali shuleni. Menyu hiyo iliyobadilishwa ya shule ina vitu 160, inajumuisha sahani za jadi za Kiukreni na sahani zingine maarufu za vyakula tofauti tofauti. [7] [8] Baraza la Mawaziri la Ukraini liliidhinisha viwango vipya vya chakula, ambavyo vilianza kutekelezwa tarehe 1 Septemba 2021. [9]

Mnamo Desemba 2019, wakati wa hotuba katika kongamano la tatu la wanawake wa Ukraini, Zelenska alianzisha kujiunga na mpango wa kimataifa wa G7 kuhusu usawa wa kijinsia, kwa ushirikiano na Biarritz, [10] ambao ulikamilishwa mnamo Septemba 2020. [11] Mnamo Novemba 2020 na Septemba 2021, Zelenska alizungumza katika kongamano la nne na la tano la wanawake wa Kiukreni, [12] [13] jukwaa linaloleta pamoja watu mashuhuri wa Kiukreni na kimataifa, wanasiasa, maafisa wa serikali, wataalamu, na viongozi wa maoni kwa haki sawa kwa wanawake . na wanaume .

Mnamo Januari 13, 2020, Volodymyr Zelensky alimjumuisha Olena kwenye bodi ya sanaa ya Art Arsenal, inayoongozwa na Waziri wa Utamaduni Volodymyr Borodiansky . [14]

Mnamo Juni 2020, Olena Zelenska alianza mpango wa kueneza lugha ya Kiukreni ulimwenguni na kuanzishwa kwa miongozo ya sauti ya lugha ya Kiukreni katika sehemu mbali mbali, haswa - katika makumbusho makubwa zaidi ulimwenguni. [15] Kama sehemu ya mpango huo, miongozo 11 ya sauti ya Kiukreni ilizinduliwa mwaka 2020 katika makumbusho ya huko Azerbaijan, [16] Austria, [17] [18] Italia, [19] [20] Latvia, Uturuki, [21] na Montenegro, [22] na vile vile katika njia mbili za basi za Lithuania . Mnamo 2021, kama sehemu ya mpango wa Zelenska, miongozo ya sauti ya lugha ya Kiukreni ilizinduliwa katika jumba la makumbusho la Mount Vernon (nyumbani kwa George Washington ), [23] [24] Makumbusho ya sanaa ya San Francisco huko California. [25]

Zelenska alizindua dodoso la pekee mnamo Mei 2020 kuhusu kuunda jamii isiyo na vizuizi, [26] kwa ushirikiano na Wizara ya mabadiliko ya kidijitali na Wizara ya Sera ya kijamii ya Ukraini . [27] Mnamo Desemba 2020, Wizara ya Mabadiliko ya Kidijitali na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraini ilisema kwamba wataunda orodha rahisi ya huduma kwa vikundi vilivyo hatarini kama sehemu ya mpango wa Zelenska wa "Bila Vikwazo", [28] utakaochapishwa kwenye tovuti ya serikali.

Olena Zelenska katika Kongamano la Tano la Wanawake wa Kiukreni

Zelenska alianzisha mkutano wa kilele wa wanawake na wanaume ulioitwa Kyiv Summit of First Ladies and Gentlemen mnamo Agosti 2021, [29] ukiwa na mada ya "Soft power in new reality".

.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Zelenska na mume wake walikuwa wanafunzi walio soma pamoja, lakini hawakufahamiana. Zelensky aliwahi kusema kwamba alijua wanafunzi wenzake wengi, lakini sio Zelenska mwenyewe. Walifahamiana baadaye sana — Zelenska alipokuwa akisoma Uhandisi wa kiraia katika Chuo Kikuu cha Kryvyi Rih National University. .

Uhusiano kati ya wanandoa hao ulikua polepole - walichumbiana kwa miaka minane kabla ya kufunga ndoa mnamo 6 Septemba 2003. Mnamo Julai 15, 2004, binti yao Oleksandra alizaliwa. Mnamo 21 Januari 2013, Zelenska alimzaa mtoto wao wa kiume Kyrylo. [30]

Zelenska alilazwa hospitalini kwa uchunguzi tarehe 16 Juni 2020 baada ya kupimwa na kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19) . [31] Ugonjwa huo ulielezewa kuwa ulikua na ukali wa wastani ambao haukuhitaji uingizaji hewa kwa mitambo . [32] Aliruhusiwa kutoka hospitalini tarehe 3 Julai 2020 na kuendelea na matibabu nyumbani. [33]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Main facts about Ukraine's next first lady Olena Zelenska". KyivPost. 24 Aprili 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "100 самых влиятельных украинцев". Focus. 23 Desemba 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "СПІКЕРИ - Олена Зеленська - Перша леді України". Ukrainian Women's Congress. Iliwekwa mnamo 1 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Prengel, Kate (22 Aprili 2019). "Olena Zelenska, Volodymyr Zelensky's Wife: 5 Fast Facts".{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Вікторія Коломієць (18 Novemba 2019). "Перша леді вирішила зайнятися реформою харчування у школах". Hromadske.TV.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Как обезопасить школьные столовые: Зеленская приглашает присоединиться к онлайн-обучению" (kwa Kirusi). Ukrinform. 20 Novemba 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-24. Iliwekwa mnamo 2022-03-14.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Презентовано План заходів з реформування системи шкільного харчування під патронатом Першої леді Олени Зеленської Archived 25 Mei 2021 at the Wayback Machine..
  8. Без цукру, солі та сосисок. Олена Зеленська та шеф-кухар Євген Клопотенко презентували оновлене шкільне меню. НВ. — 25 May 2021.
  9. Як зміниться з вересня харчування в школах: розказують Олена Зеленська та Євген Клопотенко. 1+1  — 26 May 2021.
  10. "Гендерна рівність: перша леді ініціює приєднання України до ініціативи G7 (фото, відео)". Ukrainian Independent Information Agency. 10 Desemba 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "Уряд підтримав ініціативу Олени Зеленської щодо приєднання України до «Партнерства Біарріц»". Office of the President of Ukraine. 7 Mei 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "Олена Зеленська відкрила другий день четвертого Українського жіночого конгресу". Офіс Президента України. 26 Novemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  13. "Olena Zelenska takes part in V Ukrainian Women's Congress". Office of the President of Ukraine. 16 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. "Зеленський ввів свою дружину до складу ради "Мистецького арсеналу"". РБК-Украина (kwa Kirusi). Iliwekwa mnamo 13 Januari 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. "В этом году за рубежом заработали 11 украиноязычных аудиогидов – супруга Президента" (kwa Kirusi). Укрінформ. 30 Desemba 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-03-12. Iliwekwa mnamo 2022-03-14.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  16. "У Баку запустили аудіогід українською мовою". Gazeta.ua. 25 Agosti 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  17. Дар‘я Харченко (5 Juni 2020). "В одному з найбільших музеїв Австрії з'явився україномовний гід". НВ.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  18. Костянтин Гончаров (2020-09-16). "Ще один австрійський музей "заговорив" українською мовою (відео)". УНІАН.
  19. Катерина Денісова (27 Desemba 2020). "У римському Колізеї з'явився аудіогід українською мовою". НВ.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  20. Борис Ткачук (27 Desemba 2020). "У римському Колізеї аудіогід тепер можна послухати й українською мовою". hromadske.ua.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  21. Юлія Каранковська (17 Oktoba 2020). "Повторила образ: Олена Зеленська зустрілася з першою леді Туреччини". ТСН.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  22. "В Морском музее Черногории появился аудиогид на украинском" (kwa Kirusi). Укрінформ. 2020-12-22. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-09-01. Iliwekwa mnamo 2022-03-14.
  23. "The presidential couple visited Mount Vernon where Olena Zelenska presented a Ukrainian-language audio guide". President of Ukraine - Official website. 1 Septemba 2021. Iliwekwa mnamo 2 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  24. "Володимир і Олена Зеленські презентували українськомовний гід в Музеї Джорджа Вашингтона". Ukrinform. 1 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  25. "Olena Zelenska initiates signing of memorandum on creation of Ukrainian-language audio guides with Fine Arts Museums of San Francisco". President of Ukraine - Official website. 3 Septemba 2021. Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  26. "Дружина Зеленського запросила українців до розмови". Ukrayinska Pravda. 6 Mei 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  27. Павло Калашник (6 Mei 2020). "Дружина Зеленського запросила українців на «велику розмову про безбар'єрність»". hromadske.ua.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  28. "По инициативе Зеленской в «Дії» будет раздел для незащищенных групп населения" (kwa Kirusi). Укрінформ. 2 Desemba 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-02-25. Iliwekwa mnamo 2022-03-14.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  29. "In Kyiv, the first ladies from different countries launched an international platform for solving humanitarian problems around the world". Office of the President of Ukraine. 23 Agosti 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  30. "ru:Зеленский Владимир" (kwa Kirusi). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Januari 2019. Iliwekwa mnamo 19 Agosti 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  31. Ukraine leader cancels meetings, trips after wife tests positive for coronavirus, Reuters (12 June 2020)
  32. Ukraine president's wife hospitalized with moderate COVID-19, Reuters (16 June 2020)
  33. "Zelensky's wife overcame the coronavirus, but problems remain", 3 July 2020. (uk)