Nenda kwa yaliyomo

Paulo Chong Hasang

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Paulo Chong Hasang (1794 au 1795Seoul, 22 Septemba 1839) alikuwa mmojawao Wafiadini wa Korea.[1]

Katekista huyo na wafiadini wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984[2].

Sikukuu ya Wafiadini wa Korea inaadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 20 Septemba, ila ya kwake mwenyewe ni siku ya kifodini chake, alipoteswa kikatili na hatimaye kukatwa kichwa, baada ya kuongoza Wakatoliki wa nchi hiyo kwa miaka 20 chini ya dhuluma ya serikali [3].

Mazingira[hariri | hariri chanzo]

Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu katika rasi ya Korea, nchi ya Kikonfusyo, kwa juhudi na ari za wananchi walei[4].

Mwaka 1836 Korea ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society) ambao walilisha na kuthibitisha imani kwa kutangaza Neno la Mungu na kuadhimisha sakramenti [5].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Mtoto wa mfiadini Augustino Jeong Yak-Jong na mjukuu wa mwanafalsafa Yohane Jeong Yak-Yong, ambao walikuwa kati ya Wakorea wa kwanza kuongokea dini ya Ukristo na kuandika katekisimu ya kwanza ya Kanisa Katoliki kwa Kikorea ("Jugyo Yoji").

Yakjong alipouawa pamoja na kaka wa Hasang, mke wake na watoto wengine waliachwa wakahamia vijijini. Hasang alikuwa na umri wa miaka saba.

Kisha kukua, Hasang aliajiriwa na afisa wa serikali, akapata hivyo nafasi ya kusafiri mara kadhaa hadi Beijing, alipomsihi askofu wa huko atume mapadri Korea, akamuandikia Papa Gregori XVI akimuomba aanzishe jimbo huko, jambo lililofanyika mwaka 1825.

Miaka michache baadaye, askofu Laurent-Marie-Joseph Imbert na mapadri wawili walitumwa huko. Askofu alitambua sifa za Hasang to akamfundisha Kilatini na teolojia, lakini alipotaka kumpa daraja takatifu ilizuka dhuluma dhidi ya Wakristo.

Hasang alikamatwa akampa hakimu tamko la maandishi la kutetea Ukatoliki. Kisha kulisoma, hakimu alimjibu, "Wewe uko sahihi katika yale uliyoyaandika; lakini mfalme amekataza dini hiyo, hivyo ni wajibu wako kuikataa." Hasang alijibu, "Nimekuambia mimi ni Mkristo, na nitakuwa hivyo hadi kifo changu."

Basi, Hasang aliteswa kwa namna mbalimbali bila kupotewa na utulivu wake. Hatimaye alisulubiwa akiwa na umri wa miaka 45.[6]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Roman Martyrology" (kwa Kiitaliano). The Vatican.
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/70850
  3. Martyrologium Romanum
  4. Michael Walsh, ed. "Butler's Lives of the Saints" (HarperCollins Publishers: New York, 1991), p. 297.
  5. The Liturgy of the Hours Supplement (New York: Catholic Book Publishing Co., 1992, pp. 17–18.
  6. The New Glories of the Catholic Church, (London: 1859) pp. 56-59.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.